Vyanzo vya habari nchini humo vinasema idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi na ajali zilizosababishwa na mvua kubwa ya masika imeongezeka na kufikia 125.
Jimbo la Maharashtra limekumbwa na mvua kubwa zaidi mwezi Julai katika kipindi cha miongo minne, wataalamu wanasema.
Mvua hiyo iliyodumu kwa siku kadhaa imeathiri maelfu ya watu wakati mito mikubwa iko katika hatari ya kupasuka kingo zake.
Huko Taliye karibu kilomita 180 kusini mashariki mwa mji mkuu wa kibiashara Mumbai, idadi ya waliofariki iliongezeka na kufikia 42.
Takriban watu 40 bado wamekwama na uwezekano wa kuwaokoa wakiwa hai ni mdogo kwa sababu wamenasa kwenye tope kwa zaidi ya saa 36, afisa mmoja aliyekataa kutambulishwa amesema.
Chanzo cha Habari AFP