Maoni mseto kuhusu matarajio ya wapiga kura wa Marekani kwa Rais ajaye

  • VOA News

Rais-Mteule wa Marekani Donald Trump

Donald Trump atakuwa rais wa 47 wa Marekani baadaye mwezi huu. Wapiga kura wa Marekani wana matarajio tofauti kwa rais ajaye. Mwandishi wa VOA Scott Stearns anaripoti na Khadija Riyami anaisoma ripoti kamili.

Katika jimbo la Kusini la Mississippi, matarajio kwa awamu ya pili ya urais wa Donald Trump ni mchanganyiko. Bobbie Jo Harrel alimpigia kura Trump.

Mississippi

Bobbie Jo Harrell, Mpiga Kura Mississippi anasema: “Ningependa kumuona kwa hakika akichukua udhibiti wa mpaka na hali ya wahamiaji haramu. Mimi ninachotaka ni kumsaidia kwa vyoyote nitakavyoweza, hasa pale ambapo inahusu watoto wadogo. Lakini pia ningependa kuwaona watoto wangu na wajukuu zangu wana uwezo wa kuifurahi Marekani ambayo
mimi nimekulia.”

New York

Aliyejibadilisha jinsia kutoka New York Angelo Myer ana wasi wasi kuhusu mustakbali wake chini ya utawala huo ambao umeelezea msimamo wake kwa huduma ya afya kwa wale waliobadili jinsia.
Myer, Mpiga Kura New York anasema: “Warepublican wanaangalia kutaka kujua kuhusu kuwekeza kwa watoto waliobadili jinsia kama ilivyo muhimu kuwekeza kwa watoto wao wenyewe kwasababu sisi ni kizazi kijacho nani ataiongoza hii nchi. Tuna Mawazo mazuri, na mustakbali wenye nguvu.”
Sean Cushing anamtaka Trump kulenga kwenye uchumi.
Sean Cushing, Mpiga Kura New York asema: “Akae tu kwenye ahadi zake wakati wa kampeni na kumaliza suala kodi kwenye bakhshisi kama alivyosema atafanya.”
Jeri Helton huko Mississippi anakiri kuwa uchumi ni kipaumbele cha juu.
Helton, ambaye ni Mpiga ni Kura Mississippi: “Ningependa kwa Rais Trump kuwa na uwezo wa kushusha tena gharama ya maisha kwetu sisi. Nimechoka kuishi mshahara kwa mshahara.”

Pennsylvania
Huko Pennsylvania, Sammira Cherfaoui ana wasi was kuhusu matokeo ya Trump kwahaki ya uzazi na kidini.
Sammira Cherfaoui, Mpiga Kura Pennsylvania alieleza kuwa:
“Nadhani nitapoteza haki zangu kama mwanamke. Nadhani nitapoteza haki yangu ya dini kwasababu ana kuwa anataka kuweka mbele ukristo. Naamini kuwa nchi hii iko wazi kwa kila dini. Nahisi kama vile kila mtu ni vyema awe na uwezo wa kujifunza dini akiwa shule, siyo moja tu.”

Texas

Huko Texas, mfuasi wa Trump Ross Barrera anasema ujuzi wa biashara alionao rais ajaye utamsaidia kuiweka nchi katika mwelekeo sahihi.

Barrera, Mpiga Kura Texas anasema:“Watu wamechoka. Watu wanachotaka hapa ni ajira. Wanataka uchumi mzuri.
Wanataka mfumuko wa bei ushuke. Wanataka usalama wa mipaka. Wanataka
mafuta.”
Kitu muhimu ambacho Trump anaweza kufanya kwa mpiga kura wa Mississippi ni kweka wazi ajenda yake.
Yael Frausto, Mpiga Kura Mississippi anasema: “Namtaka awe wazi kabisa kuhusu sera zake ambazo ataziweka mbele katika nchi. Ili tufahamu, kila mtu wote wa chama cha Republican na Democratic, nini wakitarajie au nini wasikitarajie katika miaka minne ijayo.”
Trump ataapishwa kama rais hapa Washington Januari 20.