Maafisa wamesema kulikuwa na majeruhi wengi katika tukio hilo la ufyatuaji risasi jumatano lakini walikataa kutoa idadi kamili.
Polisi wa Jimbo na eneo hilo wamemtaja Robert R. Card mwenye umri wa miaka 40 ambaye inasemekana wakati wa majira ya joto waliripoti kwenye kituo cha afya ya akili, kama mtu anayehusishwa na tatizo hilo.
Awali walibandika katika mtandao wa Facebook picha za mwanaume mwenye ndevu aliyevalia fulana ya kahawia na suruali ya jeans katika moja ya matukio ya eneo la uhalifu akiwa ameshikilia bunduki aina ya semi- automatic akiwa katika hali ya kufyatua risasi.
Polisi waliipata gari nyeupe aina ya SUV, wanaamini kwamba Card aliiendesha katika mji wa Lisbon, takriban kilomita 11 kusini mashariki na Sauschuck amesema watu walitakiwa kubaki ndani katika miji ya Lewiston na Lisbon.
Vyombo vya habari kadhaa vimeripoti kuwa maafisa wa usalama wa Maine walimtambua Card kama mkufunzi wa matumizi ya bunduki na mwanajeshi wa zamani wa marekani ambaye hivi karibuni aliripoti kuwa ana matatizo ya akili , pamoja na kusikia sauti . Vyokbo vya habari vimesema pia aliwahi kutishia kufyatua risasi katika eneo la Ulinzi wa Kitaifa.