Mahakama ya Marekani yatupilia kesi dhidi makampuni ya teknolojia yanayonunua madini DRC

  • VOA News

Wachimba haramu wa migodi kaika kambi ya Dark Forest Liberia

Mahakama ya rufaa ya serikali kuu ya Marekani, Jumanne ilikataa kuwajibisha  kampuni tano kubwa za teknolojia kwa madai yao ya kuunga mkono matumizi ya watoto katika shughuli za uchimbaji madini ya cobalt katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika uamuzi ulioungwa mkono na majaji wote watatu waliosikiliza kesi hiyo, Mahakama ya Rufaa ya Marekani ya Wilaya ya Columbia ilikataa kuwajibisha kampuni mama ya Google, Alphabet, Apple, Dell Technologies, Microsoft na Tesla, ikitupilia mbali rufaa ya wachimbaji madini watoto wa zamani, na wawakilishi wao.

Walalamishi walishutumu kampuni hizo tano kwa kujiunga na wauzaji bidhaa katika mradi wa "kazi ya kulazimishwa" kwa kununua kobalti, ambayo hutumiwa kutengeneza betri za lithiamu, ambazo hutumiwa sana katika vifaa vya elektroniki.

Takriban theluthi mbili ya cobalt duniani inatoka DRC. Kulingana na malalamiko hayo, makampuni hayo "yalificha kimakusudi" utegemezi wao katika ajira ya watoto, ikiwa ni pamoja na watoto wengi walioshinikizwa kuingia kazini kwa njaa na umaskini uliokithiri.

Walalamishi 16 walikuwa ni pamoja na wawakilishi wa watoto watano waliouawa katika shughuli za uchimbaji madini ya cobalt.

Lakini mahakama ya rufaa ilisema kununua kobalti katika msururu wa ugavi wa kimataifa hakufanani na "kushiriki katika mradi" chini ya sheria ya serikali kuu inayolinda watoto na waathiriwa wengine wa biashara ya binadamu na kazi ya kulazimishwa.