Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 17:45

Waziri Mkuu wa DRC Jean-Michel Lukonde ajiuzulu


Waziri Mkuu wa DRC aliyejiuzulu Jean-Michel Sama Lukonde
Waziri Mkuu wa DRC aliyejiuzulu Jean-Michel Sama Lukonde

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean-Michel Sama Lukonde, alijiuzulu siku ya Jumanne na kusababisha kuvunjwa kwa serikali yake, ofisi ya rais ilisema katika taarifa yake.

Lukonde aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Felix Tshisekedi siku nane baada ya kuthibitishwa kwa mamlaka yake kama naibu wa kitaifa. Sasa atajiunga na bunge kama mjumbe.

"Ombi lake la kujiuzulu limekubaliwa. Hata hivyo, rais ameiomba serikali (ya Lukonde) kuendelea kushughulikia masuala ya kitaifa hadi serikali mpya itakapoundwa," ofisi ya rais ilisema katika taarifa nyingine baadaye Jumanne.

Taarifa hiyo hata hivyo haikueleza sababu za Lukonde kujiuzulu.

Lukonde aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, yenye utajiri wa madini, mnamo Februari 2021.

Forum

XS
SM
MD
LG