Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:30

Wanamgambo wa ADF washukiwa kuua watu nane DRC


Wanajeshi wa Congo wakifanya doria katika kijiji cha Mwenda kufuatia shambuluo la hivi karibuni la ADF. Picha na ALEXIS HUGUET / AFP
Wanajeshi wa Congo wakifanya doria katika kijiji cha Mwenda kufuatia shambuluo la hivi karibuni la ADF. Picha na ALEXIS HUGUET / AFP

Wanangambo wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) wenye uhusiano kundi la Islamic States washukiwa kuua watu wanane katika shambulio huko mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ofisa wa wilaya hiyo amesema.

Afisa utawala Sabiti Njiamoja alisema Waasi (ADF) walikivamia kijiji cha Mayimoya kilichopo wilaya ya Beni Jumatatu jioni.

“Watu wanane wakiwemo wanawake watatu waliuawa” amesema , na kuongeza kwamba jeshi limekuwa likifanya msako katika msitu uliopo jirani.

“Tumetoa wito kwa wanajeshi wetu wachukue majukumu yao kwa sababu hivi karibuni kumekuwa na wamgambo wa ADF huko Eringeti, Kainama na Kokola” alisema ikiimanisha miji iliyopo kaskazini mwa jimbo la Kivu Kaskazini.

ADF kihistoria ni kundi la waasi wa Uganda wengi wao waislamu lililoweka ngome mashariki mwa DRC tangu mwaka 1995.

Tangu wakati huo wafuasi wake wameua maelfu ya raia, na kueneza mashambulizi kuanzia jimbo la Kivu Kaskazini hadi jimbo jirani la Ituri katika miaka ya hivi karibuni.

Shambulio la mwisho linaloshitumiwa kufanywa na kundi hilo lilikuwa Februari 6, ambapo wanakijiji 11 waliuawa katika shambulio lililofanywa katika vijiji kadhaa katika wilaya ya Mambasa katika juimbo la Ituri.

Forum

XS
SM
MD
LG