Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 20:28

Ufilipino: Maporomoko ya ardhi yaua sita, darzeni hawajulikani waliko


Waokoaji wakitoa mwili kutoka katika maporomoko ya matope huko mjini Monkayo in katika jimbo la Davao de Oro province, kusini mwa Ufilipino.
Waokoaji wakitoa mwili kutoka katika maporomoko ya matope huko mjini Monkayo in katika jimbo la Davao de Oro province, kusini mwa Ufilipino.

Mamlaka huko  kusini mwa Ufilipino wanasema watu sita wamefariki na darzeni hawajulikani  walipo baada ya maporomoko ya ardhi kutokea katika kijiji cha machimbo ya dhahabu.

Maafa hayo yametokea usiku sana Jumanne huko Masara, kijiji kimoja katika mji wa Maco katika jimbo la Davao de Oro.

Maporomoko ya ardhi yaliharibu nyumba kadhaa na kufukia mabasi mawili yaliyotumiwa kuwasafirisha wafanyakazi katika eneno la machimbo linaloendeshwa na kampuni ya Ufilipino ya Apex Mining.

Msemaji wa serikali wa jimbo anasema wafanyakazi wa utafutaji na uokoaji wanachimba kifusi kutafuta wachimba madini wasiopungua 27 ambao walikuwa katika mabasi mawili wakati maporomoko ya ardhi yalipotokea.

Wachimbaji wengine wanane walifanikiwa kunusurika kwa kuruka nje ya madirisha kabla ya mabasi hayo kufunikwa chini ya matope.

Msemaji huyo alisema jumla ya watu 46 hawajulikani waliko, japokuwa haikuwa bayana iwapo idadi hiyo inajumuisha wachimbaji 27.

Mamia ya familia karibu na Masara zimeondolewa kutoka katika nyumba zao na kupelekwa katika makazi ya dharura.

Mkoa wa kusini wa Mindanao umekumbwa na wiki kadhaa za miezi kadhaa ya mvua kubwa, lakini hali mbaya ya hewa ilipungua ilipofika Jumanne, na maporomoko ya ardhi yaliwashtua wakazi.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG