Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 22:27

Waliokuwa katika Ibada wafunikwa na maporomoko ya aridhi Ufilipino


Mwanakijiji akibeba vitu vyake baada ya maporomoko ya udongo kukikumba jijiji chake katika jimbo la Maguindanao Octoba 29, 2022. Picha na Ferdinandh CABRERA / AFP.
Mwanakijiji akibeba vitu vyake baada ya maporomoko ya udongo kukikumba jijiji chake katika jimbo la Maguindanao Octoba 29, 2022. Picha na Ferdinandh CABRERA / AFP.

Maporomoko ya aridhi yaliyosababishwa na mvua nyingi kwa siku kadhaa imefunkia nyumba ambayo watu walikuwa kwenye ibada ya Kikristo kuko Kusini mwa Ufilipino, watu kumi wakiwemo watoto watano wameuawa, Maafisa wamesema siku ya Ijumaa.

Watu wawili wamejeruhiwa, na mwanakijiji mmoja hajaonekana kufuatia maporomoko ya aridhi katika kijiji cha mbali mlimani katika mji wa madini wa Monkayo ulioko katika jimbo la Davao de Oro, mkuu wa mkoa katika ofisi ya serikali ya Ulinzi wa Raia Ednar Dayanghirang amesema.

Miili zaidi ya mitatu ilipatikana siku ya Ijumaa, baada ya juhudi za kuwatafuta watu kusitishwa Alhamisi mchana kutokana na hatari ya maporomoka zaidi ya aridhi.

“Walikuwa katika sala ndani ya nyumba hiyo wakati aridhi ilipoporomoka” Dayanghirang aliliambia shirika la habari la Associated Press kwa nji ya simu siku ya Alhamisi usiku. “Ni huzuni lakini ndiyo hali halisi iliyopo”

Watu wanaoishi jirani na kijiji hicho waliamrishwa kuondoka kutokana na wasiwasi wa aridhi - na matope kuporomoka kutokana na mvua kubwa inayoyesha bila mpangilio.

Mvua kubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa pia ilisababisha mafuriko katika vijini vilivyoko bondeni na kuwakosesha makazi watu zaidi ya 36,000 katika jimbo hilo la Davao de Oro na majimbo mengine matatu, Ofisi ya Ulinzi wa Raia imesema. Hali ya hewa imeanza kuwa shwari katika baadhi ya maeneo siku ya Ijumaa.

Angalau dhoruba 20 na vimbunga huvikumba visiwa vya Ufilipino kila mwaka, hususani nyakati za majira ya nvua ambayo huanza mwezi Juni.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG