Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 00:33

Mafuriko yanayoendelea Congo yamesababisha vifo vya watu 22


Hali ilivyo katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko nchini Congo
Hali ilivyo katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko nchini Congo

Vifo vingine vitano vilithibitishwa Jumanne pamoja na idadi ya vifo 17 vilivyoripotiwa, kulingana na John Kabeya, gavana wa jimbo la Kasai Central

Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa katikati mwa Congo yamesababisha vifo vya watu 22 wakiwemo 10 kutoka familia moja, afisa mmoja wa eneo hilo amesema Jumanne.

Mvua kubwa iliyonyesha katika wilaya ya Kananga katika jimbo la Kasai Central, iliharibu nyumba na miundombinu mingi, gavana wa jimbo hilo, John Kabeya, alisema wakati juhudi za uokoaji zikiongezeka za kuwatafuta manusura.

Vifo vingine vitano vilithibitishwa baadaye Jumanne, pamoja na idadi ya vifo 17 vilivyoripotiwa, alisema. “Kuanguka kwa ukuta kulisababisha vifo vya watu 10, watu wote wa familia moja huko Bikuku,” Kabeya alisema.

Timu ya uokozi ikiendelea na huduma kuwatafuta manusura wa mafuriko huko Congo
Timu ya uokozi ikiendelea na huduma kuwatafuta manusura wa mafuriko huko Congo

Kulikuwa na uharibifu mkubwa wa vifaa uliosababishwa na mafuriko, kulingana na Nathalie Kambala, mkurugenzi wa Kanda wa The Hand in Hand for Integral Development, shirika lisilo la kiserikali. Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa yanashuhudiwa mara kwa mara katika maeneo ya Kongo, hasa katika maeneo ya ndani kabisa.

Mwezi Mei, zaidi ya watu 400 walifariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha, katika jimbo la Kivu Kusini, huko mashariki mwa Congo.

Forum

XS
SM
MD
LG