Katika uamuzi wake Jumanne Jaji Chacha Mwita ameruhusu kesi hiyo kuendelea.
Gashagua anatarajia kusimama mbele ya bunge la taifa katika Seneti ambako mashitaka dhidi yake yatasikilizwa.
Gashagua amesisitiza kwamba jaribio la kutaka kumuondoa madarakani lina ushawishi wa kisiasa na kueleza kujiamini kwake kwamba mahakama itatoa maamuzi ya haki.
Mawakili wa Gashagua, Paul Muite na Tom Macharia Jumatatu walimuuliza Jaji Chacha Mwita kutoa amri kusimamisha kesi ya Gashagua.
Katika hatua ya kihistoria wiki iliyopita, Bunge la kitaifa la Kenya lilipiga kura kwa wingi kumshitaki Gashagua kwa tuhuma 11 zikiwemo za ufisadi.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 59 amekanusha tuhuma na ataendelea kuhudumu katika nafasi yake hadi pale seneti itakapoamua kupitisha kuondolewa kwake.
Gashagua alifungua kesi kulizuia bunge la taifa kuendelea Jumatano na Alhamisi akisema kutaka kuondolewa kwake siyo haki na kumeharakishwa sana.