Uamuzi wa Mahakama ya Juu hiyo umefutilia mbali sheria ya Uingereza ya kikoloni ambayo ilikuwa ina wabagua wanawake.
Jopo la majaji watano wa mahakama ya juu kwa pamoja walitoa uamuzi kuwa kosa hilo la mtu kuwa na mahusiano na mwanamke mwengine nje ya ndoa bila ya ridhaa ya mumewe imepitwa na wakati na ina wanyang'anya wanawake uhuru wao.
Uzinifu hauwezi na hautakiwi kuwa uhalifu,” Jaji Mkuu Dipak Misra amesema wakati akisoma hukumu hiyo.
Mfanyabiashara Joseph Shine aliitaka mahakama hiyo kufutilia mbali sheria hiyo, kwa hoja ya kuwa ilikuwa inawabagua wanawake na haingii akilini.
Katika uamuzi wake, mahakama hiyo imesema kuwa mahusiano nje ya ndoa ni suala binafsi kati ya watu wazima na bado ni sababu inayokubalika kupelekea talaka.
Uzinzi bado unaendelea kuwa ni uhalfiu katika nchi nyingi za Asia, kama ilivyo katika baadhi ya majimbo ya Marekani.