Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria katika baraza la seneti la bunge la Marekani, Charles Grassley alimpatia saa kadhaa hadi Jumamosi mchana mwanamke anayemshutumu Brett Kavanaugh, mtu aliyeteuliwa kuchukua nafasi katika mahakama ya juu Marekani kwa shambulizi la ngono kuamua kama mwanamke huyo atatoa ushahidi wiki ijayo, kulingana na ripoti ya gazeti la New York Times.
Gazeti hilo liliripoti kuwa Grassley alituma barua pepe kwa mawakili wa Christine Blazey Ford, iliyosema kuwa jopo la baraza la seneti lazima lipate uamuzi wa Ford kutoa ushahidi ifikapo Jumamosi mchana.
Grassley alitangaza ongezeko la muda kupitia Twitter katika hali ya kuomba msamaha iliyomlenga kavanaugh. "Jaji kavanaugh mimi Charles kama mwenyekiti wa kamati ya sheria kwenye baraza la seneti nimeongeza muda kwa Dr.Ford kuamua kama anataka kuendelea na taarifa aliyoitoa wiki iliyopita ili atoe ushahidi kwa seneti na tuweze kusonga mbele. Kama mwenyekiti wa jopo hili ninataka kusikia pia kutoka upande wake.Ninatumai unaelewa hili".