Maelfu ya wanawake watarajiwa kuandamana Jumamosi Washington

FILE - People listen to speeches at the Women's March in opposition to the agenda and rhetoric of President Donald Trump in Washington, Jan. 21, 2017.

Maelfu ya wanawake watakusanyika katika miji mikubwa mbalimbali Marekani na duniani kote Jumamosi kwa maandamano ya kila mwaka yanayo fanyika kwa mara ya tatu yakishinikiza haki sawa za kijinsia na kutaka dunia itafakari juu ya wasiwasi ulioko juu ya uharibifu wa mazingira na suala la haki za wahamiaji, kati ya vitu vingine vingi.

Maandamano haya yanayo fanywa na wanawake yalianza kufanyika mwaka 2017, siku moja baada ya Donald Trump kuapishwa kuwa rais wa Marekani.

Siku ya kwanza kamili ya utawala wa Rais Trump, mamia ya maelfu ya wanawake waliteremka jijini Washington kuonyesha upinzani wao mkubwa dhidi ya utawala mpya na sera zake.

Maandamano kama hayo pia yalifanyika katika maeneo zaidi ya 600 ndani ya Marekani na duniani kote kuunga mkono maandamano yaliyokuwa yanafanyika mjini Washington.

Peter Newsham, kaimu mkuu wa polisi Washington kwa wakati huo, alisema kuwa maandamano hayo katika mji mkuu wa Marekani, “ni msongamano mkubwa hadi hivi sasa na hakuna hata nafasi tena ya kuandamana.”

Wengi wa wanawake hao walikuwa wamevaa kofia zilizofumwa katika umbile la “paka”, ikiwa na masikio madogo yap aka, kuonyesha kuunga mkono hisia zilizoko dhidi ya Trump na kukosoa maoni ya Trump yenye lugha chafu aliyokuwa ameyatoa miaka kadhaa huko nyuma kabla ya kuingia katika medani ya siasa.