Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 03:25

Trump akejeli maadamano ya Jumamosi


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump Jumapili amekejeli kitendo cha maelfu ya watu waliojitokeza kushiriki katika maadamano katika miji mikuu mbalimbali Marekani kupinga utawala wake mpya.

“Nimeangalia maandamano hayo jana lakini nilipata hisia kwamba tulikuwa na uchaguzi!” Trump alisema katika ujumbe wake wa Twitter kutoka ikulu ya White House, makazi yake kwa miaka minne ijayo. “Kwa nini watu hawa hawakupiga kura?"

”Mwanaharakati wa haki za wanawake Gloria Steinem,

Mwanaharakati Gloria Steinem mwenye skafu nyekundu
Mwanaharakati Gloria Steinem mwenye skafu nyekundu

muimbaji mashuhuri Madonna, mwigizaji Scarlett Johansson na masupasta wengine waliongoza maadamano ya wanawake Jumamosi huko Washington DC kupinga kuapishwa kwa Trump kuwa rais wa 45 wa Marekani Ijumaa.

Saa mbili baadae, Trump amesema katika ujumbe mwingine waTwitter, “Maandamano ya amani ni ushindi wa demokrasia yetu. Hata kama sio kila wakati nakubaliana, lakini natambua haki ya watu kutoa maoni yao.”

Trump pia amesifia idadi kubwa ya watu walioshuhudia kuapishwa kwake katika televisheni, akisema, “ Wow, tathmini ya kwenye televisheni imetoka: watu milioni 31 waliangalia sherehe za kuapishwa, milioni 11 zaidi ya tathmini nzuri iliyotolewa miaka 4 iliyopita!”

Tathmini iliyofanywa na kituo cha televisheni cha Nielsen imesema watu milioni 30.6 waliotizama kuapishwa kwa Trump kuingia madarakani ambayo imeipita idadi ya watu milioni 20.6 walioangalia kuapishwa kwa rais wa zamani, Barack Obama katika awamu ya pili ya utawala wake 2013.

Hata hivyo idadi ya walioangalia kuapishwa kwa Trump ilipungua kwa asilimia 19 ya idadi ya watu milioni 37.8 walioangalia sherehe za kwanza za kuapishwa Obama mwaka 2009.

Kawaida wamarekani wengi wanaangalia sherehe za kuapishwa marais na idadi kubwa kuliko zote ya tathmini za watu kuangalia sherehe hizo ilikuwa watu- milioni 41.8- iliyosajiliwa mwaka 1981 wakati Rais Ronald Reagan alipoapishwa katika awamu ya kwanza kati ya awamu mbili za utawala wake.

XS
SM
MD
LG