Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 03:42

Maandamano dhidi ya rais mteule Trump yafanyika Marekani


 Waandamanaji wakipita katika mtaa wa 57th Street mjini New York wakilekea hadi jengo la Trump Tower, Nov. 9, 2016.
Waandamanaji wakipita katika mtaa wa 57th Street mjini New York wakilekea hadi jengo la Trump Tower, Nov. 9, 2016.

Maandamano ya kumpiga rais mteule wa marekani Donald Trump yanafanyika katika karibu miji saba ya Marekani siku moja tu baada ya ushindi wake kwenye uchaguzi ulokua na ushindani mkubwa katika historia ya karibuni ya taifa hili.

Maelfu ya watu wanaandamana New York, Chicago, Washington na miji mingine mitano Jumatano usiku ili kupinga kauli za kudhalilisha za rais mteule Trump aliyokua anatoa wakati wa kipndi cha kampeni za uchaguzi mkuu.

Donald Trumpakikubali ushindi wake akiwa hoteli ya Hilton jijini New York City, Nov. 9, 2016.
Donald Trumpakikubali ushindi wake akiwa hoteli ya Hilton jijini New York City, Nov. 9, 2016.

Wengi wamekua na mabango yanayolaani matamshi yake ya kuwapinga wahamiaji, waislamu na makundi mengine mbali mbali.

Akitoa hotuba yake ya kukubali ushindi Jumanne usiku huko New York, Trump alitoa wito kwa taifa kuungana na kufanya kazi pamoja.

"Sasa ni wakati kwa wamarekani kutibu majeraha ya mgawanyiko na tunabidi kuungana tena. Kwa warepublican, wademokrat na wasioegemea upande wowote kote nchini ninasema wakati umefika kwetu sisi kuungana na kuwa watu wa pamoja."

Wito huo unaonekana haujakubaliwa na Wamarekani wote kwani Jumatano usiku waandamanaji walikusanyika pia mbele ya White House wakitoa wito wa kukomeshwa ubaguzi wakati Trump anajitayarisha kuchukua madaraka ya nchi hii.

Barack Obama
Barack Obama

Mapema Jumatano, Rais Barack Obama akizungmza Ikulu, alitangaza kwamba amekaribisha Trump Alhamisi huko Ikulu ili kuanza kujadili kipindi cha mpito na kukabidhiana madaraka kama ilivyo utamaduni wa demokrasia ya Marekani na kutoa wito kwa wamarekani kuungana pamoja nyuma ya rais wa 45.

"Kwa hivyo nimeagizia timu yangu kufuata mfano wa timu ya rais Bush miaka minane iliyopita na kufanya kazi kwa bidi kuhakikisha kipindi cha mpito cha rais mteule kinafanikiwa kwa sababu sisi sote tunamtakia ufanisi katika kutuunganisha na kuiongoza nchi hii."

Maneneo hayo ya umoja yalitolewa pia naHillary Clinton wakati wa asubuhi baada ya kukubali kushindwa.

Clinton alisema taifa limegawika lakini bado anaimani na na misingi ya Marekani na hivi sasa watu wakubali kwamba Trump ndiye rais wa taifa hilo kuu.

Matamshi hayo yote yanaonekana hayakuwaridhisha baadhi ya wamarekani wenye hasira kwani walishuka mitaana kuandamana dhidi ya ushindi huo ambao haukutazamiwa.

Waandamanaji wakiwa katika mtaa wa Fifth Avenue nje ya jengo la Trump Tower, New York.
Waandamanaji wakiwa katika mtaa wa Fifth Avenue nje ya jengo la Trump Tower, New York.

Huko Austin Texas wanafunzi wa chuo kikuu cha Austin waliandamana hadi bunge la jimbo wakibeba mabango yanayosema "yeye si rais wangu."

Mjini Nashville wanafunzi wengine wengi weusi wamekua wakisema wamechoshwa na ubaguzi na wanastahiki kupata maisha bora zaidi.

Maandamano mjini New York na Washington na Chcago yanafanyika mbele ya majengo ya Trump, yakifanyika kwa amani huku polisi wakihakikisha usalama usalama unadumishwa.

XS
SM
MD
LG