Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yafanyika Marekani, Ulaya

Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump wakihudhuria sherehe ya Siku ya Mashujaa, New York, Novemba 11, 2019. (AP Photo/Andrew Harnik)

Mataifa yaliyoungana kumaliza vita vya kwanza vya dunia yanaadhimisha miaka 101 Jumatatu, tangu kutiwa saini makubaliano ya kumaliza vita hivyo na Ujeruimani.

Trump

Rais wa Marekani Donald Trump akizungumza katika paredi maalum ya kuadhimisha siku ya mashujaa huko New York, Novemba 11, 2019.

Wakati huohuo Marekani imeadhimisha miaka 100 ya mashujaa wake waliopigana katika vita vya dunia na vita vingine.

Huko Ufaransa rais Emmanuel Macron aliongoza sherehe za makumbusho kwenye uwanja wa Arc de Triomphe.

Nchini Uingereza watu walikaa kimya kwa dakika mbili katika viwanja vyote vya makumbusho, huku waziri mkuu Boris Johnson akiongoza sherehe za kitaifa

Sherehe za kuadhimisha siku hiyo zimefanyika pia katika nchi 10 kuu zilizoungana kupambana na Ujerumani ili kumaliza vita hivyo ikiwa ni pamoja na Marekani, India, Sri lanka, poland Rashia na Australia.