Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 00:28

Trump awaenzi mashujaa katika makaburi ya Arlington


Mwanajeshi wa Jeshi la Majini akipita na mtoto wa kike katika makaburi ya mashujaa waliokufa katika Vita vya Kwanza vya Dunia katika siku ya Mashujaa, huko Ufaransa, Mei 27, 2018.
Mwanajeshi wa Jeshi la Majini akipita na mtoto wa kike katika makaburi ya mashujaa waliokufa katika Vita vya Kwanza vya Dunia katika siku ya Mashujaa, huko Ufaransa, Mei 27, 2018.

Marekani inaadhimisha Siku ya Mashujaa leo Jumatatu. Rais Donald Trump ameweka shada la maua katika Kaburi la Mwanajeshi Asiyejulikana huko katika Makaburi ya Kitaifa Arlington.

Siku ya Mashujaa ilianza mwaka 1865, mara tu baada ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe, wakati kundi la watumwa waliokuwa huru walipoadhimisha kile kinachojulikana kama kumbukumbu ya kwanza ya wale waliokufa katika vita vya taifa.

Kundi hilo lilifukuwa miili ya zaidi ya wanajeshi wa Muungano 250 kutoka katika kaburi la pamoja katika jela ya muungano wa kitaifa huko Charleston, South Carolina, na kuwapa maziko yanayostahili.

Kwa zaidi ya miaka 50, sikukuu hiyo ilikuwa inawakumbuka tu wale waliouwawa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini, na siyo vita nyingine za Marekani.

Ni pale baada ya Marekani kuingia katika Vita ya Kwanza ya Dunia ndipo Siku ya Mashujaa ilipo wahusisha wale wote waliokufa katika vita zote.

Wamarekani wengi hupata mapumziko katika siku hii kwa kutoenda kazini au shuleni. Siku tatu za mapumziko mwisho wa wiki zinajulikana kama ni kipindi kisichokuwa rasmi cha kuanza msimu wa mapumziko katika kipindi cha joto. Familia nyingi huandaa pikiniki au kutembelea fukwe za bahari, mbuga au maeneo ya kuweka kambi.

Siku ya Mashujaa rasmi inaadhimishwa siku ya Jumatatu ya mwisho ya Mwezi Mei, imetengwa kwa ajili ya kuwaenzi wanajeshi wote waliokufa katika vita ikiwa ni sehemu ya historia kote nchini Marekani. Bunge la Marekani lilitangaza Siku ya Mashujaa kuwa ni mapumziko ya kiserikali kitaifa mwaka 1971.

Siku ya Jumapili, tukio linalojulikana kama Rolling Thunder, ambapo maelfu ya wanajeshi wastaafu na wengine wakiwa wamepanda pikipiki, wamemiminika Washington kama wanavyofanya kila mwaka, wakipita katika maeneo ya kumbukumbu katika viwanja vya National Mall kuwaenzi wanajeshi wa Marekani waliokufa wakiwa wanatumikia taifa katika vita nchi za nje. Mlio wa pikipiki zao husikika katika umbali wa kilomita kadhaa, kabla ya kuonekana.

XS
SM
MD
LG