Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:20

Ujumbe wa Marekani uko Korea Kaskazini kuandaa mkutano wa Trump, Kim


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Kikundi cha maafisa wa serikali ya Marekani wamevuka mpaka wa Korea Kaskazini Jumapili kuanza kufanya matayarisho ya mazungumzo kati ya Rais Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, kwa mujibu wa gazeti la Washington Post.

Gazeti hilo, limemkariri mtu aliyekuwa na uzoefu wa matayarisho hayo, akisema kuwa Balozi wa zamani wa Marekani Korea Kusini Sung Kim ameitwa kutoka katika kituo chake cha Kazi huko Ufilipino kuja kuongoza matayarisho hayo.

Rais Donald Trump amesema jioni Jumamosi kuwa maandalizi kwa ajili ya mkutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yaliyopangwa kufanyika Juni 12 huko Singapore yako katika mpangilio huo na maelezo zaidi juu ya mkutano huo yanaendelea kufanyiwa kazi.

Mazungumzo hayo “yanaendelea vizuri sana,” amesema Trump

XS
SM
MD
LG