Kyiv yataka mkutano wa haraka na Russia

Chancela wa Ujerumani Olaf Scholz (kushoto) akutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy mjini Kyiv

Kyiv imeomba ufanyike mkutano wa haraka na Russia kujadili hatua ya Moscow kuweka wanajeshi wengi na vifaa vya jeshi karibu na Ukraine na ndani ya Crimea ambako wamejiingiza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema Jumapili jioni kwamba Moscow haijajibu baada ya Kyiv Ijumaa kutoa ombi hilo kupitia Taasisi ya Usalama na Ushirikiano ya ulaya- OSCE.

Kyiv imeitaka Russia kuelezea vitendo vyake hivyo dhidi yake, ikisema sasa inataka mkutano ufanyike ndani ya saa 48.

Maelezo ya Kuleba yanakuja kabla ya kurudiwa juhudi za kidiplomasia zenye lengo la kuzuia uvamizi wa Russia ambapo umesababisha khofu, huku chansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa kwenye mji mkuu wa Ukraine Jumatatu kwa ajili ya mazungumzo kufuatia mzozo na rais Volodymyr Zelensky.

Mawaziri wa fedha wa kundi la G7 la nchi zenye uchumi mkubwa duniani wameionya Russia kuwa itakabiliwa na athari kubwa za kiuchumi kama itaivamia Ukraine na wameahidi kusaidia uchumi wa baadae wakati wa shambulizi.

Nchi zinazounda G7 ni Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Japan, Uingereza na Marekani.