Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:37

Biden awataka Wamarekani kuondoka Ukraine


Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito kwa Wamarekani wote waliobakia nchini Ukraine kuondoka nchini humo haraka.

Biden ameeleza hatua hii ni kutokana na vitisho vinavyoongezeka vya hatua za kijeshi za Russia.

Rais amesema hata tuma vikosi kuwaokoa Wamarekani kama Moscow itaivamia Ukraine.

Ameonya kuwa mambo yatakuwa mabaya haraka katika eneo hilo.

Russia imeendelea kukanusha kuhusu mipango yoyote ya kuivamia Ukraine licha ya kupeleka wanajeshi zaidi ya laki moja karibu na mpaka.

Lakini imeanza mazoezi makubwa ya kijeshi na nchi Jirani ya Belarus.

Ukraine imeshutumu Russia kwa kuziba njia kuingia kwenye bahari.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema Alhamisi Ulaya inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kiusalama ambao haujawahi kutokea katika miongo kadhaa kufuatia mivutano hiyo.

XS
SM
MD
LG