Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:47

Rais wa Ufaransa afanya ziara Ukraine.


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Rais wa ufaransa Emmanuel Macron amekwenda Ukraine Jumanne kwa ajili ya mazungumzo na rais VOLODYMYR ZELENSKYY kutokana na mivutano kati ya Russia na Ukraine.

Ziara yake inakuja siku moja baada ya kumpongeza Zelenskyy kwa kujizuiya binafsi alioonyesha wakati akikabiliwa na maelfu ya wanajeshi wa Russia kwenye mpaka wa nchi yake.

Akizungumza baada ya saa kadhaa za mazungumzo na rais wa Russia Valadmir Putin mjini Moscow , Macron pia alisisitiza haja kwa ulaya kufanya kazi na Russia kutafuta njia na uwezo wa kujenga ushirikiano wa Pamoja kama watu wa ulaya.

Hata hivyo katika mvutano uliopo Russia imekanusha mara kadhaa kwamba ina mpango wa kumvamia jirani yake Ukraine, lakini inataka Marekani na washirika wake kuizuiya Ukraine na mataifa mengine yaliyokuwa ta umoja wa Soviet kujiunga na muungano wa NATO. Marekani na NATO wamekataa matakwa hayo.

XS
SM
MD
LG