Mwandishi wa sauti ya Amerika Elzabeth Lee amegundua kwamba si kila mtu aliyempigia kura Trump anajichukulia kuwa ni Mrepublikan na sio Warepublikan wote wanaojichukulia ni waungaji mkono wa Trump.
Kutokana na kuwepo kwa kiongozi mpya White House Warepublican kote nchini wanatafakari juu ya jinsi utawala wa Trump ulivyomalizika kwa kishindo na watarajiye nini katika siku zijazo.
Chris Morris ni mhamiaji kutoka Jamaica, msimamizi wa ujenzi katika mji wa Haymarket Virginia karibu km 65 kutoka mahala waandamanaji walivamia majengo ya bunge mjini Washington hapo Januari 6. Alimpigia kura Trump lakini anasema kile kilichotokea kwenye majengo ya Bunge si jambo linalokubalika.
Chris Morris Msimamizi wa Ujenzi Virginia :"Kwa wale waliovamia jengo la bunge , mimi ninadhani wengi wao walifanya hivyo kwa sehemu kubwa kwa ajli ya Trump, ili kumunga mkono, na yeye amesababisha nchi yetu kugawika.
Wademocrats wanamtuhumu Trump kwa kuchochea na kuhamasisha uvamzi wa jengo la bunge, akiwa anaendelea kudai bila ya ushahidi kwamba ameibiwa kura.
Morris anakubaliana na Warepublican wachache waliopiga kura ya kumfungulia mashtaka Trump.
Chris Morris, msimamizi wa ujenzi Virginia : "Ninadhani walikua hawajafurahia kumona mtu aliyekua na nafasi hiyo muhimu kutowajibika na majukumu ya uraisi."
Na mmoja kati ya wajumbe hao ni Liz Cheney, aliye wasababisha Warepublican kupiga kura jana katka kikao chão cha faragha iwapo wamtowe kutoka nafasi yake kama kiongozi wa wabunge wa Republican kwenye Baraza la Wawakilishi.
Liz Cheney, mwenyekiti wa Warepublican katika Baraza la Wawakilishi : "Ahsanteni sana, kiongozi wa wachache, kiongozi wetu, kwa hakika tulikuwa na upigaji kura muhimu leo usku . ulikuwa wakati mzuri jioni ya leo tukipanga yale ambayo tunabidi kufanya kuelekea mbele, na kueleza bayana kwamba hatutagawika."
Wafuasi wa chama cha Republican wamegawika kama wabunge wao juu ya masuala hayo lakini Cristina Morcom wa Texas anaona kuna mambo yanayo fanana kati ya malalamiko mbele ya majengo ya bunge na maandamano ya wanaopinga ubaguzi, Black lives matter, ambapo baadhi ya waandamanaji walitumia fursa hiyo kusababisha ghasia.
Christina Morcom mkazi wa texas : "Watu wale wote, wafuasi wa Trump au walovaa kama wafuasi wa trump walitaka kuchafua sifa za marepublicans. Ninadhani kila kitu kinawezekana kutokana na nyakati tunaoishi hii leo."
Maoni yanayo tofautiana kumhusu Trump na ghasia kwenye Capitol ina mulika jinsi taifa lilivyogawika na kuongeza uwezekano wa chama cha Republican kugawika. Hata hivyo kwa jumla wengi wao wanaamni maseneta wasimhukumu Trump kuwa na hatia kwani uamuzi huo unaweza kuligawa taifa zaidi.