Kremlin yasema kuna uwezekano ndege aliyokuwemo Prigozhin iliangushwa kwa makusudi

A view shows the grave of Russian mercenary chief Yevgeny Prigozhin in St Petersburg

Kremlin imesema Jumatano wachunguzi walikuwa wanaangalia uwezekano wa ndege iliyokuwa imembeba kiongozi wa mamluki Yevgeny Prigozhin kwamba iliangushwa kwa makusudi ikiwa ni  tathmini ya kwanza kuwa inawezekana ameuwawa.

“ ni dhahiri kwamba mitazamo tofauti inazingatiwa ikiwa ni pamoja na kwamba unajua tunazungumzia kuhusu ukatili wa makusudi,” msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu uchunguzi huo.

Alipoulizwa kama shirika la kimataifa la usafiri wa anga lingechunguza ajali hiyo, Peskov alisema kuwa mazingira yamekuwa tofauti ingawa alionya kuwa wachunguzi bado hawajafanya hitimisho rasmi kuhusu kile kilichotokea.

tusubiri matokeo ya uchunguzi wa Russia,’ alisema Pescov. Ndege ya binafsi ya Embraer ambayo Prigozhin alikuwa akisafiria kwenda St petesrsburg kutoka Moscow ilianguka kaskazini mwaka Moscow na kuuwa watu wote 10 agosti 23, Wakiwemo viongozi wengine wajuu wa wagner , walinzi wanne wa Prighozhin na wafanyakazi watatu.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.