Hofu hiyo ilienea pale kimbunga hicho kilipoanza kupiga sehemu za kati na mashariki ya nchi na kusababisha vifo vya watu watatu.
Serikali ya Cuba imefungua vituo vya kuwapatia hifadhi watu na kujaribu kuzuia uharibifu mkubwa wa mimeya ya miwa na cacao kabla ya kimbunga kuwasili nchini humo Jumapili.
Wengi kati ya waliyohamishwa walipelekwa kwa jamaa zao baadhi wakiwekwa kwenye vituo hivyo vya serikali.
Mamia ya watu wanaoishi kwenye maeneo ya milimani walikimbilia ndani ya mapango wakisubiri kimbunga kipita.
Kituo cha kufuatilia vimbunga hapa Marekani, NHC, kinasema kimbunga Elsa kilikuwa kina kasi ya kilomita 95 kwa saa kilipopita sehemu za mashariki ya Cuba na kimekuwa kikipungua nguvu Jumatatu.