Mamlaka ya Kitamil Nadu na jirani Andhra Pradesh walitoa tahadhari kubwa, mamlaka katika majimbo yote mawili yakionya wavuvi dhidi ya kujitosa baharini kwa uvuvi.
Uwanja wa ndege wa Chennai ulisimamisha shughuli zake kwa saa mbili Jumatatu asubuhi baada ya mvua kubwa kunyesha jijini, ripoti za vyombo vya habari zilisema, na safari kadhaa za ndege zilikatishwa au kuelekezwa katika miji mingine.
Kimbunga Michaung kinatarajiwa kutua kwenye ufukwe wa Andhra Pradesh siku ya Jumanne asubuhi, kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa nchini huku kukiwa na upepo mkali unaovuma kwa kasi ya kilomita 110 kwa saa.