Kenya lazima ichukue hatua kudhibiti mioto shuleni, wasema mzazi na manusura

Sehemu ya bweni likiwa limeshika moto katika shule ya msingi ya Hillside Endarasha, Nyeri, Kenya, Sept. 6, 2024.

Wakenya wanasema janga hilo baya limesababisha kwa mara nyingine haja ya haraka wa kuimarisha hatua salama katika shule nchini humo.

Shule ya Endarasha Hillside Academy iliungua septemba 6 na kuchoma bwenila wanafunzi wakati watoto wa kiume walikuwa wamelala. Vyombo vya habari vya ndani vimesema waathirika waliungua vibaya sana na kushindwa kutambuliwa.

Hili lilikuwamoja ya tukio baya zaidi la moto kwa kiasi kikubwa lilihusisha vurugu za wanafunzi, ambazo zimerekodiwa kwa miaka mingi na mamlaka.

Mwaka 2017 moto uliwashwa na mwanafunzi katika shule ya sekondari ya Moi na kusababisha vifo vya wanafunzi wenzake 10. Baadae msichana huyo aliyesababisha moto alikutwa na hatia ya kuuwa bila kukusudia.

Katika kumbukumbu ya matukio ya majanga ya kibinadamu ya kusikitisha , Mwihaki Mwangi ameliambia shirika la habari la Roita kwamba binti yake mwenye umri wa miaka 14 , Bubbles alifanikiwa kuepuka moto katika shule ya wasichana ya MOI lakini alirudi kwa ujasiri kuwakoa marafiki zake lakini yeye hakunusurika.

Hata hivyo wambui Kigwa aliyenusurika na Moto bado anakumbuka ajali hiyo.

Mwambui Kigwa alinusurika katika moto mwaka 2017 aneleza: "Nilihisi uoga mkubwa sana na kukosa tumaini kwa sababu moshi unapokukaba hujui njia ya kutokea, ilikuwa inatisha na ilitisha zaidi ikizingatiwa kwamba hatujaandaliwa mapema endapo hali hiyo inapotokea unatakiwa kufanya nini , unatakiwa kuruka na sio kutembea kwenye moto , hatukuandaliwa kabisa kuhusu kitu kama hicho."