Kauli ya Ruto ya kuwashutumu watumishi wa mahakama yazua hasira Kenya

Rais William Ruto wa Kenya baada ya kuzungumza na waandishi wa habari huko Karen Agosti 17, 2022. Picha na Patrick Meinhardt / AFP

Rais wa Kenya William Ruto amezua hasira baada ya kuwashutumu baadhi ya watumishi wa mahakama kuchukua rushwa kazini wakati wapinzani wake wakijaribu kuzuia baadhi ya sera za serikali.

Rais Ruro ambaye alichaguliwa mwaka 2022, kwa ahadi ya kupunguza ugumu wa maisha kwa Wakenya wa kawaida, ilikuwa ni kampeni yake ya kupunguza deni la taifa, na “matumizi mabaya” ya serikali katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki yenye watu wapatao milioni 53.

Mipango kadhaa ya kodi na mpango wa ubinafsishaji uliozinduliwa na serikali kwa ajili ya kufanya mageuzi mbali mbali ya kiuchumi imezuiliwa na mahakama baada ya changamoto za kisheria mwaka jana.

“Haiwezekani kuwa tunaiheshimu mahakama (wakati) watu wachache wanaofaidika na rushwa wanawatumia maafisa wa mahakama kuzuia miradi yetu ya maendeleo” alisema Ruro katika hotuba yake ya Jumanne.

“Sisi ni demokrasia, tuna heshimu, na tutaulinda, uhuru wa Mahakama” alisema “kitu ambacho hatutakiruhusu ni dhulma na kutokujali kwa mahakama.”

Matamshi yake yamezua ghadhabu katika sekta ya sheria, huku jaji mkuu Martha Koome akionya hatari ya “machafuko” iwapo uhuru wa mahakama hauta heshimiwa.

Chama cha wanasheria nchini Kenya kimeitisha maandamanao ya nchi nzima wiki ajayo.

Chanzo cha habari hii ni DShirika la habari la AFP