Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:00

Washukiwa wa mauaji ya Mwanariadha Kenya wafikishwa mahakamani


Benjamin Kiplagat akimaliza mbio za wanaume za mita 3000 wakati wa mashindano ya Olimpiki huko Rio mwaka 2016. Picha na Fabrice COFFRINI / AFP
Benjamin Kiplagat akimaliza mbio za wanaume za mita 3000 wakati wa mashindano ya Olimpiki huko Rio mwaka 2016. Picha na Fabrice COFFRINI / AFP

Washukiwa wawili wamefikishwa makahamani siku ya Jumanne nchini Kenya kwa tuhuma za mauaji ya mawanariadha wa Uganda Benjamin Kiplagat ambaye alikutwa amefariki mwishoni wiki akiwa na jeraha la kuchomwa kisu shingoni.

Mahakama ya hakimu katika mji wa Eldoret huko Rift Valley imetoa amri kuwa washukiwa hao wawili waendelee kubaki rumande kwa siku 21 ili kuiwezesha polisi kuendelea na uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanariadha huyo wa mbio za kuruka vizuizi mwenye umri wa miaka 34.

Washukiwa hao, waliotambuliwa kwenye nyaraka za mahakana ni David Ekhai Lokere (alias Timo) mwenye mri wa miaka 25, na Peter Ushuru Khalumi, mwenye mri wa miaka 30.

Mwili wa Kiplagat uligundulika katika barabara nje ya mji wa Eldoret majira ya alfajiri siku ya Jumapili akiwa na jeraha la kisu shingoni.

Wakati sababu za maujai hayo hazijulikani, polisi wamesema upepezi unaonyesha kuwa Kiplagat alikuwa “ameviziwa” na wanaume wawili kabla ya kuigonga ikipiki yao kwenye gari la Kiplagat.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG