Mamlaka ya Ushindani ya Mdhibiti wa Kenya siku ya Jumanne ilitangaza faini hiyo, ambayo ni rekodi ya juu katika taifa hilo la Afrika Mashariki, ikisema MAF Kenya ilikuwa na hatia ya kuwapa wasambazaji bidhaa wawili wa ndani masharti yasiyofaa.
Majid Al Futtaim ina imani kamili katika usawa na uadilifu wa mazingira yetu ya biashara na inakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mamlaka ya Ushindani kampuni hiyo ilisema katika taarifa.
Katika kufikia uamuzi wake mamlaka ilipuuza ukweli kwamba wasambazaji hao wawili wa ndani walikuwa tayari wameondoa malalamiko yao na kutia saini mikataba mipya na mfanyabaishara huyo MAF ilisema katika taarifa yake.
Forum