Uhusiano wa Fatah Sharif na kundi la Hamas huenda ukaongeza matatizo ya UNRWA ambalo tayari lina upungufu wa ufadhili wa dola milioni 80 mwaka huu. Wakosoaji wamerejea kuikosoa idara hiyo wakisema kuwa haikuwa ikifanya vya kutosha kuwaondoa wanachama wa Hamas miongoni mwa wafanyakazi wake.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukiichunguza UNRWA tangu Januari mwaka huu baada ya Israel kudai kuwa wafanyakazi wake 12 walihusika kwenye shambulizi la Oktoba 7 dhidi yake ambako watu 1,200 walikufa huku wengine 250 wakitekwa. Madai hayo yalipelekea nchi zaidi ya darzeni moja kusitisha ufadhili wao kwa UNRWA na kusababisha upungufu wa takriban dola milioni 450 kwa shirika hilo.
Hamas limesema kuwa Sharif aliuwawa pamoja na mke wake, na mtoto mmoja wa kike na wa kiume, kwenye shambulizi la anga katika kambi ya wakimbizi ya Al Buss, moja wapo ya kambi 12 zinazotoa hifadhi kwa wakimbizi wa Palestina, karibu na mji wa kusini wa Tyre.