Kabila aliongoza Kongo kutoka mwaka wa 2001 hadi 2019, kabla ya rais wa sasa Felix Tshisekedi, kuchukua uongozi wa nchi hiyo.
Wiki iliyopita, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, alisema Kabila aliruhusu wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF), kundi ambalo lina uhusiano na Kundi la kigaidi la Islamic State (IS), kujenga kambi kubwa, na pia kuchimba dhahabu na kuuza mbao, kati ya shughuli zingine za kiuchumi.
"Madai ya uongo ya Rais Museveni, ambaye ni mmoja wa wahalifu wakuu katika eneo hilo, ni kejeli tu, na yanalenga kuwavuruga watu wa Kongo na kuwagawanya," Kabila alisema katika taarifa yake kwa shirika la habari la Reuters.
Kundi la ADF, ambalo lilianzishwa mwaka 1996, awali ilikuwa kundi la waasi wa Uganda, wakifanya mashambulizi katika eneo la Rwenzori magharibi mwa nchi hiyo.
Waasi hao hatimaye walifurushwa na kufukuzwa na waliobakiia, walivuka mpaka na kuingia katika misitu ya mashariki mwa Kongo ambako wamepata hifadhi.