Juhudi za uokoaji Afrika Kusini zaendelea huku usalama wa waliokwama katika mgodi ukiwa mashakani

Polisi wa Afrika Kusini South wakiwa wamelizunguka tundu la mgodi ambako mamia ya wachimbaji wamekwama huku juhudi za uokoaji zikiendelea.

Jeshi la polisi Afrika kusini -SAPS na maafisa wa jeshi wamesema juhudi za uokoaji kwa ajili ya wachimbaji madini waliokwama chini ya ardhi zinaendelea huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama wa maisha yao.

Zaidi ya wachimbaji haramu 1000 tayari wametoka katika wiki za hivi karibuni wakati polisi wakiendelea na msako, angalau mwili mmoja wa mtu aliyekufa umeletwa juu ya ardhi . Mamia wanaaminika bado wamekwama chini ya ardhi kwenye shimo lenye kina cha zaidi kilomita 2.

Taasisi za kiraia zinaowawakilisha wale waliobaki katika machimbo ya Stilfontein zimesema wachimbaji hao wako tayari kutoka , lakini operesheni za polisi zinaongeza muda wao wa kuchimba, jambo ambalo katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini

Afrika Kusini, Zwelinzima Vavi ameelezea kuwa ni sawa na kifo cha taratibu.

Msemaji wa SAPS Brigedia Athlenda Mathe alisisitiza nia yao ya dhati ya uokoaji. “mamlaka yetu iko wazi, ni kuzuia na kupambana na uhalifu na bado tunaona kwamba kinachoendelea huko chini ni uhalifu mtupu. Shughuli ya uokoaji inaendelea, alisema Mathe katika mahakama kuu ya Pretoria.