Ivory Coast inaendelea kukumbwa na mvutano wa kisiasa

  • Abdushakur Aboud

A young man throws a tire onto a fire during a protest by supporters of opposition leader Alassane Ouattara in Abidjan, 03 Dec 2010

Melfu ya wafuasi wa Bw Alassane Outtara walimiminika katika mitaa ya Abidjan Jumatatu, na kuchoma moto magurudumu ya magari wakimtaka Laurent Gbagbo kuacha madaraka. Wakati huo huo, rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki ananedelea na juhudi za kutanzua mzozo wa kisiasa.

Guillaume Soro, kiongozi wa zamani wa waasi, aliyekuwa waziri mkuu chini ya rais Gbagbo aliteuliwa Jumapili na Bw Outtara kuongoza serikali mpya.Huku Gbagbo amemteuwa mchumi Gilobert Marie N'gbo Ake kuwa waziri mkuu wake na kuunda serikali mpya.

Katika mahojiano na redio ya Ufaransa Europe 1, Soror amesema kamba serikali ya Outtara inatafuta suluhisho la amani kwa mzozo huo lakini waasi hawatakua na njia nyingine isipokua kuanza vita ikiwa Gbagbo hatoacha madaraka.

Amesema wamemuambia Gbagbo wako tayari kufanya kazi naye ikiwa atakubali kuacha madaraka kwa amani.

Wachambuzi wa kisiasa wanahofu mvutano huo unaweza kupelekea vita nchini humo. Akizungumza na sauti ya Amerika, Mwesiga Beregu wa chuo kikuu cha Dar es-Salaam anasema ni lazima kuchunguza kilichosababisha kutokea mzozo huo kabla ya kuupatia suluhisho.