Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:07

ECOWAS: Lazima Gbagbo amkabidhi Outtara madaraka


Laurent Gbagbo, katikati, akisimama mbele ya baraZa lake jipya la mawaziri.
Laurent Gbagbo, katikati, akisimama mbele ya baraZa lake jipya la mawaziri.

Baada ya mkutano wao wa Abuja, mji mkuu wa Nigeria, viongozi wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, wamemtaka rais Laurent Gbagbo kumkabidhi madaraka Alassane Outtara, mshindi wa matokeo ya uchaguzi wa rais huko Ivory Coast, ambayo yaliidhinishwa na Umoja wa Mataifa.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, mwenyekiti wa zamu wa ECOWAS, alisema Jumatano kwamba viongozi wenzake wa zamani wamemtaka Bw. Gbagbo akabidhi madaraka bila ya kuchelewa kwa sababu alishindwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Rais Jonathan alisema, “Wanaamini kwamba katika uchaguzi wa kidemokrasia kura za wananchi lazima zitiliwe maanani. ECOWAS haitokubali tena demokrasia ya bandia, na wanaamini matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi na kukubaliwa na mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast ni ya kweli na ya haki na kwamba Outtara ndiye mtu wanae muunga mkono kama rais wa Ivory Coast”.

Licha ya uwamuzi huo inaonekana Bw. Gbagbo hatobadili msimamo wake, naye waziri wake mpya wa mambo ya kigeni ametishia kumfukuza mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG