Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast ameapishwa Jumamosi kwa mhula mwengine wa miaka mitano, licha ya upinzani mkubwa kutoka wananchi na viongozi wa dunia wanaosema mshindi wa kweli ni mgombea wa upinzani Alassane Outtara.
Rais Gbagbo aliapishwa katika sherehe zilizotangazwa na televisheni ya taifa siku moja baada ya Mhakama ya Katiba ya Ivory Coast kubadilisha matokeo yaliyotangzwa na tume ya uchgauzi yanayompatia ushindi Bw Outtara.
Mkuu wa majeshi Jenerali Philipe Mangou alitangaza kwenye televisheni ya Taifa siku ya Ijuma kwamba jeshi liemahidi kumunga mkono Gbagbo.
Viongozi wa Dunia, akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, Rais Barack Obama na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy wamemtambua Bw Outtara kama rais mteule wa Ivory Coast na kutoa wito kwa Bw Gbagbo kukubali matokeo hayo.