Italia yaiomba UN kuchunguza mauaji ya balozi wake

Waziri Luigi Di Maio

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia ameuomba Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi kuhusiana na mauaji ya balozi wake nchini DRC katika shambulizi la kushtukiza.

Mwana Diplomasia Luca Attanasio, mwenye umri wa miaka 43, aliuwawa siku mbili zilizopita baada ya msAfara wa magari ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, kushambuliwa mashariki mwa nchi karibu na mpaka wa Rwanda.

Waziri Luigi Di Maio mapema leo amelihutubia Baraza Kuu la Bunge nchini Italy kuhusiana na shambulizi hilo la DRC ambalo pia liliua dereva na mlinzi wa balozi Attanasio.

Tumeiomba rasmi WFP pamoja na Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kilichotokea, sababu za mikakati ya kiusalama iliyowekwa pamoja na waliofanya maamuzi. Tumeeleza kuwa tunatarajia majibu ya kina kwa haraka.

Matamshi ya Di Maio yamekuja baada ya miili ya balozi Luca Attanasio na mlinzi wake kurejeshwa mjini Rome kwa ndege ya kijeshi.

Wabunge walimpongeza Di Maio kabla ya hotuba hiyo ikiwa ishara ya heshima kwa balozi aliyeuwawa. Di Miao amesema kuwa limekuwa jambo la kuvunja moyo kupokea milli hiyo kwenye uwanja wa ndege.



//Luigi di Maio, Waziri wa mambo ya kigeni wa Italy//

Ulikuwa wakati mgumu kwetu sisi kupokea miili ya wazalendo hao waliokufa kutokana na shambulizi la kikatili tukiandamana na waziri mkuu pamoja na wanafamilia. Ni tukio la kuvunja moyo sana.//


//Narrator//

Rais wa DRC Felix Tshisekedi aliitembelea familia ya Attanasio wakati akiahidi kuwa yeye mwenyewe atahusika katika kumaliza mauwaji yanayoendelea mashariki mwa taifa hilo.


//Felix Tshisekedi, Rais wa DRC//

Sasa hivi kipaumbele changu ni kuhusika katika kuangamiza ukatili huu zaidi ya nilivyo fanya hapo awali.//


//Narrator//

Wachunguzi wa Italy pamoja na wale kutoka Umoja wa Mataifa wanatarajiwa katika Jamhuri ya kidemokeasia ya Congo hivi karibubi ili kutanzua kuchhunguza mauwaji hayo.