Iran yazidisha juhudi za kuwasaka wanawake wasiovaa hijab

  • VOA News

Maandamano nchini Iran.

Maafisa wa serikali ya  Iran wanawaweka wanawake chini ya uangalizi mkubwa ili kutekeleza masharti ya  kuvaa hijabu kwa lazima, hata ndani ya magari.

Baadaye wanatoa adhabu, ikiwa ni pamoja na kutwaa magari ambayo wanawake wanaokiuka kanuni hizo, wanatumia, shirika la kimataifa la kutetea haki, Amnesty International lilisema Jumatano.

Uongozi wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu ulitikiswa mwaka 2022 na maandamano makubwa yaliyoshuhudia wanawake wakishutumu kanuni za mavazi lakini umeweka wazi kuwa hauna mpango wa kuachana na sharti la vazi la lazima la hijabu lililowekwa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.

Amnesty ilisema katika ripoti, iliyotokana na "mapitio ya nyaraka rasmi" na ushuhuda kutoka kwa wanawake zaidi ya 40 ndani ya Iran iliyochapishwa kabla ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake ya Machi 8, kwamba wanawake walikuwa wakilengwa na "uchunguzi mkubwa" katika maeneo ya umma na " ukaguzi wa polisi" unaolenga madereva wanawake.