Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka yawaachilia maelfu ya wahamiaji San Diego

Watu wakisubiri kuomba hifadhi katika eneo la Bandari ya San Isidro, mpaka wa Mexico na San Diego, June 1, 2023, in Tijuana, Mexico.

Idara ya forodha na ulinzi wa mipaka ya Marekani mwezi uliopita imewaachilia maelfu ya wahamiaji kwenye mitaa ya  San Diego.

Idadi hiyo ni pamoja na takriban wengine 1,000 katika mji wa pwani wa Oceanside, baada ya kuzidiwa na rekodi ya idadi ya wanaotafuta hifadhi kutoka duniani kote.

Lakini sasa , huku rekodi ya wanaowasili ikiwa kubwa, kuachiliwa huko kunafanyika mara kadhaa kwa siku na hivyo wastani wa watu 550 wanaingia mitaani kwa siku, kulingana na kituo cha sheria cha watetezi wa wahamiaji.

Makundi ya kibinadamu ya misaada na watu wanaojitolea wanawakaribisha wahamiaji na kuwasaidia kufikia mwisho wa safari yao kwingineko Marekani, lakini pia kuwapa mahitaji muhimu kama vile vyakula vya moto , na wakati mwingine makazi ya muda.

Mara nyingi kuachiliwa huku mitaani kunatokea San Yidro, wilaya ya San Diego ambayo inapakana na mji wa Mexico wa Tijuana, lakini pia kunafanyika katika vitongoji kama vile Oceanside na ElCajon mashariki mwa San Diego.