Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:44

Maombi ya wahamiaji walioingia kupitia mpaka wa Marekani na Mexico kukataliwa


Wahamiaji waliovuka mpaka kuingia Marekani kutoka Mexico wakisubiri katika ukuta wa mpaka wa Marekani ambako wako walinzi wa Marekani wa mpakani katika eneo la Ciudad Juarez, Mexico, Alhamisi, Machi 30, 2023.
Wahamiaji waliovuka mpaka kuingia Marekani kutoka Mexico wakisubiri katika ukuta wa mpaka wa Marekani ambako wako walinzi wa Marekani wa mpakani katika eneo la Ciudad Juarez, Mexico, Alhamisi, Machi 30, 2023.

Marekani Alhamisi itaanza kuwakatalia maombi ya hifadhi  wahamiaji ambao waliingia kupitia mpaka wa marekani na mexico kabla ya kwanza kuomba kwa njia ya  mtandao au  kuomba kwanza katika nchi waliyopitia kuingia Marekani.

Sheria hiyo mpya inawakilisha mabadiliko makubwa jinsi marekani inavyoshughulika na wanaotafuta hifadhi ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi mpakani kwa kutarajia wiki hii ni mwisho wa masharti yanayojulikana kama Tittle – 42.

Janga la COVID-19 Lilipelekea masharti yaliyoruhusu maafisa wa mpakani kurejesha haraka watu na waliofanya hivyo mara milioni 2.8 tangu Machi 2020.

Lakini baada ya masharti hayo kumalizika kwa muda wake Alhamisi, wahamiaji waliokamatwa wakivuka mpaka hawataruhusiwa kurejea kwa miaka mitano na wanaweza kukabiliwa na mashtaka ya jinai ikiwa watafanya hivyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani Alejandro Myorkas anaeleza: “Wacha mimi niwe wazi kuhusu kuondolewa kwa masharti ya Tittle- 42, haimaanishi kwamba mpaka wetu upo wazi."

Anafafanua zaidi: "Kwa kweli ni kinyume chake. Matumizi yetu ya mamlaka ya utekelezaji wa uhamiaji chini ya kifungu cha nane cha kanuni za Umoja wa Mataifa inamaanisha hatua kali zitachukuliwa kwa watu wanaovuka mpaka kinyume cha sheria. Tofauti na tittle -42 mtu atakayeondolewa chini ya kifungu cha nane anakabiliwa na angalau marufuku ya miaka mitano kuingia tena Marekani na anaweza kushitakiwa kwa makosa ya jinai ikiwa atajaribu kuvuka tena."

XS
SM
MD
LG