Waziri wa mambo ya nje wa China, Qin Gang amesema ni muhimu kuleta utulivu wenye uhusiano kati ya China na Marekani baada ya mfululizo wa maneno na vitendo potofu vilivyorudisha nyuma uhusiano wa nchi hizo.
Katika mkutano uliofanyika Beijing kati yake na balozi wa Marekani nchini China Nicholas Burns, Qin alisisitiza Marekani lazima irekebishe namna inavyoshughulikia suala la Taiwan na kukomesha kufichwa kwa kanuni ya “China Moja”.
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani ulidorora mwaka jana wakati spika wa baraza la wawakilishi wa wakati huo Nancy Pelosi alipofanya ziara rasmi Taiwan na kuikasirisha China ambayo inadai kisiwa hicho kama eneo lake.