Kituo hicho katika mji wa Mexico wa Ciudad Juarez kilikuwa kinawahifadhi wanaume 68 kutoka Amerika ya kati na Amerika kusini, ambalo ni eneo kuu la kuvuka mpaka kwa wahamiaji au waomba hifadhi wanaotaka kuingia Marekani.
Waliofariki na kujeruhiwa ni kutoka Guatemala, Honduras, El Salvador, Venezuela, Colombia na Ecuador.
Waziri wa mambo ya nje wa Guatemala Mario Bucaro alisema 28 kati ya waliokufa ni raia wa Guatemala.
Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador alisema wahamiaji waliposikia kuwa watarudishwa katika nchi zao kutoka Mexico, walianza kuchoma moto ndani ya kituo hicho kupinga kurudisha makwao.