Hotuba ya Hali ya Taifa : Baada ya kufunguliwa mashtaka, unatarajia nini katika hotuba ya Rais Trump?

Rais Donald Trump alipotoa hotuba yake ya Hali ya Taifa katika Bunge la Marekani, mjini Washington, huku Makamu wa Rais Mike Pence na Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi, Mdemokrat wakisikiliza, Jumanne Februari 5, 2019 (AP Photo/Andrew Harnik)
 

Rais Washington - Alianzisha utamaduni huo katika mji wa New York kwa hotuba fupi kwa kipimo cha hivi leo; kwa kweli ilikuwa hotuba fupi ya Hali ya Taifa kuliko zote baadae, ikiwa na maneno 1,089.

Rais Lincoln alikuwa na kazi ngumu mnamo Disemba 1862 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, alipowasilisha hotuba yake ya Hali ya Taifa katika Bunge. Wiki 10 kabla, alikuwa ametoa Tamko la kuwaachia watumwa katika maeneo ambayo bado yalikuwa yanashikiliwa na wanaopinga kuunganisha taifa.

Rais Roosevelt - Mnamo mwaka 1941, baada ya muongo moja wa kutetereka kwa uchumi alizungumzia vitu vinne muhimu vya uhuru wa binadamu - "Uhuru wa kusema na kujielezea," " Uhuru wa kila mtu kumuabudu Mungu kwa njia anayotaka," " Uhuru wa kupata wanachotaka," na "Uhuru wa kutoishi kwa hofu."

Rais Johnson - Huu ulikuwa mwaka ambapo juhudi za 'Kupambana na Umaskini' na juhudi hii iliingizwa katika miswada iliyosaidia kuanzisha programu ambazo zipo hadi hivi leo, ikiwemo msaada wa chakula, Msaada wa matibabu inayojulikana kama Medicaid, Medicare na Title I

Rais Ford - Hotuba yake ya kwanza ya Hali ya Taifa ilikuwa wakati mgumu, ilifuatia kujiuzulu kwa Rais Richard Nixon.

Rais Obama - Hotuba yake mwisho ya Hali ya Taifa ilitoa matumaini baada ya miaka 8 ya kutumikia wadhifa huo na nchi ikiimarika baada ya mgogoro wa kifedha wa 2007.

Hotuba yake ya Hali ya Taifa inakuja baada ya kesi ya jaribio la kumuondoa madarakani kufanyika.