Mpango huo wa awamu 3 kwa ajili ya eneo la Palestina uliwasilishwa mwishoni mwa mwezi na Rais wa Marekani Joe Biden, na unasimamiwa na wapatanishi wakuu Qatar na Misri, unalenga kumaliza vita, pamoja na kuachiliwa huru kwa takriban mateka 120 wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas.
Afisa mwingine wa Palestina anayefahamu kuhusu pendekezo hilo la sitisho la mapigano amesema kuwa maafisa wa Israel wapo kwenye mazungumzo na Qatar. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa mashauriano yataendelea wiki hii, ingawa hajatoa maelezo zaidi kuhusu muda.
Kundi la Hamas ambalo linadhibiti Gaza limeondoa pendekeo kuu ambalo linaitaka kwanza Israel kuweka nia ya dhati ya sitisho la kudumu la mapigano, kabla ya kusaini makubaliano. Afisa wa Palestina anayehusika kwa karibu kwenye mazungumzo hayo amesema kuwa pendekezo huenda likapelekea muundo wa mkataba kama litakubaliwa na Israel na huenda likamaliza vita.