Hali mpya ya hatari kudhibiti COVID-19 yatangazwa Tokyo

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga ametangaza rasmi hali mpya ya hatari huko Tokyo kutokana na kuongezeka kwa kesi mpya za COVID-19 katika mji huo mkuu.

Amri hiyo mpya itaanza kutumika Jumatatu ijayo, Julai 12 hadi Agosti 22 - kipindi chote cha muda wa Olimpiki ya Tokyo, ambayo itafanyika kati ya Julai 23 na Agosti 8.

Hali mpya ya au kuwazuia kabisa.tahadhari inaweza kusababisha serikali ama kupunguza idadi ya watazamaji wanaoruhusiwa kushuhudia hafla za Olimpiki mpaka watu 5,000,

Waandaaji wa Olimpiki ya Tokyo walitangaza mwezi uliopita kwamba watawaruhusu watu 10,000 tu, au asilimia 50 ya uwezo wa ukumbi, katika hafla zote licha ya wataalam wa afya kuishauri serikali kuwa kupiga marufuku watazamaji wote ilikuwa chaguo lenye hatari ndogo zaidi katika michezo hiyo.

Watizamaji wa kigeni tayari wamekatazwa kuhudhuria michezo hiyo ya Olimpiki.

Thomas Bach.

Maafisa wa serikali wa eneo na wa kitaifa pamoja na maafisa wa Olympiki watafanya uamuzi wa mwisho Alhamisi au Ijumaa iwapo waruhusu watizamaji baada ya kukutana na Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Thomas Bach.

Bach aliwasili Tokyo Alhamisi na mara moja aliingia katika karatini ya lazima ya siku tatu.

Tokyo na mikoa mengine kadhaa ilitoka katika hali ya tahadhari kamili iliyokuwa imewekwa tangu Aprili na vivi sasa ziko katika hali ya tahadhari ya kiasi ambayo itamalizika Jumapili 11.

Hata hivyo, Japan inaendelea kukabiliana na wimbi la nne la maambukizi mapya na kampeni ya kuchanja inayoenda polepole na hadi sasa ni raia wa Japan asilimia 15 ndio waliopatiwa chanjo kamili. Tokyo iliripoti maambukizi 920 mapya Jumatano, ikiwa ni idadi ya juu zaidi tangu mwezi Mei.