Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephene Dujarric ameambia wanahabari Jumanne kuhusu barua ya Guterres, kutokana na misuada miwili iliopitishwa Jumatatu na bunge la Israel la Knesset. “Kwa hakika iwapo itatekelezwa, ni dhahiri kuwa itakuwa na athari kubwa kwenye hali ya kibinadamu kwa Wapalestina kwenye maeneo yaliokaliwa,” Dujarric amesema. Ameongeza kusema kuwa Guterres pia ameandika barua kwa mkuu wa Baraza Kuu la UN ambalo lilibuni shirika la UNRWA linalosaidia Wapalestina, Desemba 1949.
Guterrea hapo nyuma alikuwa amekosoa sheria hizo ambazo zimepangwa kutekelezwa baada ya siku 90, akisema kuwa zitakuwa na athari kubwa kwa wakimbizi wa Kipalestina. Guterres pia amesihi Israel kushikilia majukumu yake chini ya sheria za kibinadamu za kimataifa, akisema kuwa sheria za kitaifa haziwezi kuwa juu yazo. Mjumbe wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa Danny Danon amesema kuwa shirika la UNRWA limekuwa likisaidia Hamas, suala ambalo huenda Guterres halioni.