Waziri huyo, Cecilia Abena Dapaah ambaye alijiuzulu mwezi Julai anachunguzwa kwa tuhuma za rushwa baada ya kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kugunduliwa nyumbani kwake, kulingana na mwendesha mashtaka huyo maalum.
Uchunguzi ulianza baada ya wafanyakazi wake wa nyumbani kudaiwa kuiba fedha taslimu zaidi ya dola milioni 1.3 kutoka nyumbani kwa waziri huyo wa mazingira.
"Uchunguzi huu kimsingi unalenga kuangalia mali zao na miamala ya kifedha ndani ya Marekani," iliandika ofisi ya Mwendesha Mashtaka Maalum siku ya Jumatano kwenye mtandao wa X, ambayo zamani ilikuwa Twitter.
"Juhudi hizi za ushirikiano ili kuhakikisha uhalali wa utajiri wa Bi Dapaah na washirika wake, katika muktadha wa fedha zao zilizosafirishwa kutoka Ghana kwenda Marekani na kinyume chake."
Mawakili wa waziri huyo wa zamani walikataa kujibu ombi la shirila la habari la AFP kutoa maoni yao.
Akaunti za Dapaah tangu wakati huo zimezuiwa na mwendesha mashtaka maalum, ambaye anashughulikia kesi za ufisadi zinazowahusu maafisa wa umma, majaji au wanachama wakuu wa chama cha siasa.
Chanzo cha habari ni Shirika la habari la AFP