Akizungumuza na makamanda wa jeshi la Congo FARDC, mkuu wa jeshi la Uganda UPDF Jenerali Kainarugaba Muhoozi amesema Uganda hainabudi kushirikiana na Congo kwani ni majirani, ndugu na marafiki wa muda mrefu.
Amesema ushirikiano ni lazima kwa nchi hizo mbili kwani zinalazimika kuwalinda raia wao dhidi ya mashambulizi ya kundi la kigaidi la ADF.
Alisisitiza kwamba uwamuzi huu ni ishara kwamba nchi hizo za Kiafrika zinauwezo wa kuumaliaza mgogoro wao bila ya msaada kutoka nje.
Mkuu wa jeshi la Congo, Jenarali Christian Tshiwewe Songesa aliwapongeza Marais Felix Tshiskedi wa Congo na Yoweri Museveni wa Uganda kwa kuanzisha ushirikiano huo mpya baada ya Uganda kumteua kamanda mpya wa jeshi lake.
“Tunapaswa kuunga mkono juhudi za viongozi wetu kwa kuweka majeshi yetu ya mataifa mawili pamoja kupambana na adui wetu ADF anae waua raia wetu, nakushurukuru kwa uteuzi wako kuwa kiongozi mpya wa jeshi la Uganda,” amesema Jenerali Tshiwewe.
Kabla ya makubaliano hayo jeshi la Uganda limekuwa likishutumiwa katika wilaya Rutshuru kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, jambo ambalo Uganda daima limekuwa likikanusha.
Mkutano huo wa kijeshi umefanyika wakati waasi wa kundi la M23 wameweka ngombe yao mpakani mwa Congo na Uganda katika mji wa Bunagana na kufanya biashara katika wilaya za Kisoro na Kampala huko Uganda ili kuweza kukidhi mahitaji ya kila siku ya wanamgambo wake wakati wakipamaba na jeshi la serikali ya DRC katika wilaya ya Rutsuru, Nyiragongo na Masisi karibu na mji wa Goma.
Imetayarishwa na Austere Malivika, Sauti ya Amerika, Goma.