Makadirio ya kiasi hicho cha pesa ni kulingana na taarifa za maafisa wa ujasusi na takwimu za wizara ya kazi na usimamizi wa biashara ndogo ndogo. Taarifa hiyo ni kulingana na Roy Dotson msimamizi wa idara ya kitaifa ya kurejesha mali zilizopotea kwa njia ya ulaghai wakati wa majanga.

Maafisa hawakujumuisha kesi za ulaghai kuhusiana na janga la corona ambazo tayari zimefikishwa mahakamani na wizara ya haki. Kesi nyingi zinatokana na ulaghai wa watu kudai mafao kwa vile hawana ajira.
Wizara ya kazi imeripoti kwamba karibu dola bilioni 87 huenda zililipwa kimakosa kwa watu waliodai kwamba hawakuwa na ajira idadi kubwa ya madai hayo yakiwa ya ulaghai. Maafisa wa ujasusi walisema kwamba wamekamata kiasi cha dola bilioni 1.2.
Uchunguzi unaendelea kuhusu pesa zilizotolewa kwa watu waliodai kutokuwa na ajira sawa na ulaghai kupitia kwa mikopo.