Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 15:18

Dola bilioni 100 kwa ajili ya Covid zimeibiwa Marekani


Watu waliopoteza kazi kutokana na janga la Corona wakiwa wamepanga foleni katika kituo cha ajira, Fort Smith, Arkansas, Marekani. April 6, 2020. PICHA: REUTERS/Nick Oxford/Maktaba
Watu waliopoteza kazi kutokana na janga la Corona wakiwa wamepanga foleni katika kituo cha ajira, Fort Smith, Arkansas, Marekani. April 6, 2020. PICHA: REUTERS/Nick Oxford/Maktaba

Karibu kiasi cha dola bilioni 100 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kusaidia biashara na watu waliopoteza kazi kutokana na janga la virusi vya Corona nchini Marekani, zimeibiwa.

Makadirio ya kiasi hicho cha pesa ni kulingana na taarifa za maafisa wa ujasusi na takwimu za wizara ya kazi na usimamizi wa biashara ndogo ndogo.

Taarifa hiyo ni kulingana na msimamizi wa idara ya kitaifa ya kurejesha mali zilizopotea kwa njia ya ulaghai wakati wa majanga Roy Dotson.

Maafisa hawakujumulisha kesi za ulaghai kuhusiana na janga la corona, ambazo tayari zimefikishwa mahakamani na wizara ya haki.

Kesi nyingi zinatokana na ulaghai wa watu kudai mafao kwa vile hawana ajira.

Wizara ya kazi imeripoti kwamba karibu dola bilioni 87 huenda zililipwa kimakosa kwa watu waliodai kwamba hawakuwa na ajira, idadi kubwa ya madai hayo yakiwa ya ulaghai.

Maafisa wa ujasusi wamesema kwamba wamekamata kiasi cha dola bilioni 1.2.

Uchunguzi unaendelea kuhusu pesa zilizotolewa kwa watu waliodai kutokuwa na ajira, sawa na ulaghai kupitia kwa mikopo.

Kiasi cha dola bilioni 2.3 zimerejeshwa baada ya ushirikiano kati ya maafisa wa serikali na benki uliopelekea pesa zilizokuwa zimetolewa kurejeshwa kabla ya kutumika.

Zaidi ya kesi 900 za uhalifu kuhusiana na pesa zilizotolewa wkaati wa janga la Corona, zinachunguzwa katika kila jimbo.

Watu 100 wamekamatwa kufikia sasa.

XS
SM
MD
LG