Mamlaka zimepongeza mafanikio ya usalama tangu mzozo ulipozuka mwezi Julai, tume ya haki za binadamu iliyoteuliwa na serikali imesema Jumatatu.
Mapigano kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa ndani ambao wanaishutumu serikali kwa kulitenga eneo hilo limekuwa mgogoro mkubwa zaidi wa usalama nchini Ethiopia tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili katika eneo jirani la Tigray mwaka mmoja uliopita.
Takriban watu 183 wameuwawa mwezi wa kwanza wa mzozo huo umoja wa mataifa umesema mwishoni mwa mwezi August. Lakini kutokana na mtandao wa internet kuwa chini kwenye eneo hilo , imekuwa vigumu kupata picha kamili ya hali ilivyo.
Katika ripoti mpya , tume ya haki za binadamu ya Ethiopia imeandika matukio kadhaa kuhusu mauaji ya raia mwezi huu. Ripoti hiyo imedai kwamba vikosi vya serikali vimefanya mauaji ya kiholela dhidi ya raia waliokamatwa mitaani au katika msako wa nyumba hadi nyumba baada ya kuwatuhumu kutoa taarifa au silaha kwa wanamgambo hao.